MAKALA

CHAKULA BORA NA NAFUU CHA SAMAKI NI SULUHISHO LA UHAKIKA KWA MAENDELEO YA UFUGAJI SAMAKI TANZANIA

20/10/2017

Chakula cha samaki ni tatizo kubwa katika maendeleo ya ufugaji wa samaki hapa nchini. Wengi wa wafugaji wadogo wa samaki hutegemea kurutubisha bwawa kwa kutumia chakula kisichokuwa na ubora kulisha samaki. Matumizi ya chakula duni husababisha kudumaa na kupungua kwa thamani ya samaki ambapo hukatisha tamaa watu wengi kuweza kujitosa katika kazi hii ya ufugaji wa samaki. Juhudi za kuendeleza chakula cha asili cha samaki ni muhimu sana kwani chakula bora na nafuu husaidia kupunguza gharama za uzalishaji, na hivyo kuvutia wawekezaji binafsi na wa kibiashara katika ufugaji na hatimaye kuongeza uzalishaji wa samaki. Iwapo chakula cha samaki chenye kiwango kinachokubalika kitapatikana kwa urahisi katika jamii, wanakaya wanaweza kukipata kwa gharama ndogo, na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji na hivyo kuongeza kipato cha mfugaji. Hii itatatua si tu tatizo la upatikanaji wa chakula lakini pia ufugaji wa samaki utakuwa chanzo cha kuaminika kwa shughuli za kuongeza kipato kwa wafugaji na pia kwa wazalishaji wa chakula cha samaki. Kwa kuongezea, mfumo wa ufugaji utaimarisha uwezeshwaji wa wanawake na kutoa fursa ya ushiriki wao kiuchumi kwanipamoja na kazi nyingine za nyumbani, wanawake huwajibika siku hadi siku katika mabwawa yaliyopo kwenye makazi yao.

Hivi sasa kuna Mradi aunaotekelezwa na kwa pamoja na watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA). Mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Lengo kuu la Mradi ni kutengeneza chakula cha samaki chenye ubora na nafuu kwa kutumia bidhaa zinazopatikana katika maeneo waliko wafugaji. Utafiti wa awali uliofanyika ulikuwa na lengo la kupata maarifa na maoni ya watu wa vijijini katika masuala ya kulisha samaki na usimamizi wa bwawa, kuweka kumbukumbu ya ulishaji wa chakula katika mabwawa,desturi ya kulisha samaki katika maeneo husika pamoja na kutambua mazao yanayopatikana katika maeneo hayo. Utafiti ulifanywa katika wilaya tatu ambazo ni Songea, Mufindi, na Mvomero. Malighafi zilikusanywa na kufanyiwa tathmini ya lishe na kutengenezewa mkokotoo wa chakula cha samaki kule Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro. Katika malighafi hizo palikuwepo na majani ya mihogo, maharage, nazi, samaki, damu ya mifugo, mbegu za keki ya alizeti, karanga, mahindi, mchele, majani ya maboga, unga wa mihogo, moringa, majani ya mipapai pamoja na viazi vikuu. Malighafi hizo ambazo hupatikana kwa urahisi katika wilaya hizo zilitumika kutengenezea aina saba za vyakula vilivyotumika kwa majaribio kwa miezi sita kuangalia ukuaji wa samaki na kubainisha ufanisi na unafuu wa gharama za chakula kulingana na malighafi zilizotumika.

​Jumla ya vifaranga 250 vya samaki vilifugwa katika ndoo ishirini (20) kwa ajili ya majaribio na samaki wakubwa waliwekwa kwenye visiba kumi na viwili (12) vya saruji TAFIRI Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia ukuaji wa muda mrefu kama sehemu ya kwanza ya majaribio. Sehemu ya pili ya majaribio itafanyika katika mashamba ya wafugaji wa samaki waliochaguliwa kutoka Wilaya za Songea na Mufindi. Wafugaji wa samaki waliochaguliwa kutoka katika wilaya hizi mbili tayari wameshapata mafunzo kwa ajili ya kulisha samaki na usimamizi wa mabwawa. Majaribio yote yatafanyika kwa usimamizi wa karibu wa Maafisa Uvuvi wa Wilaya ili kuhakikisha kwamba panakuwa na usimamizi mzuri. Baada ya kukamilika kwa mradi inatarajiwa kwamba kutakuwa na ubora wa hali ya juu wa chakula cha samaki chenye unafuu kwa ajili ya ufugaji endelevu wa Perege katika nchi yetu. Kwa hiyo utafiti huu utachangia katika kutatua tatizo la upatikanaji wa chakula bora na nafuu cha samaki na hivyo kuchangia katika maendeleo ya ufugaji wa samaki pamoja na kuongeza usalama wa chakula na kipato kwa jamii.

NAILAH ABDUL 5/11/2016 03:21:33 PM 11/05/2017 03:21:33 AM
Nashukuru kwa chakula cha samaki elekezi hata hivyo jinsi ya kuchanganya hayo mazao ni muhim ukanieleza ili nitengeneze mwenyewe. Reply
SAILALE 11/05/2016 03:41:37 AM
Vyema, Nailah, je unafuga samaki gani na utafugia wapi, ili tukupe msaada wa kiutalaam Reply
FRED MRAMBA 08/06/2016 10:29:44 AM
Mimi ni mfanyabiashara Ila naitaji kufanya biashara ya samaki eneo la kuwafugia ipo nipo mwanza Reply
MOOCHA R.G 02/09/2017 17:03:44 PM
Mimi ni mfugaji wa samaki kutoka mkoa wa mbeya wilaya ya mbeya vijijini,nafuga samaki aina ya magege au huku wanaita sato na kambale napenda kujua namna ya kuchanganya chakula na mixing ratio hasa kwa raw materials zinazopatikana kwa urahisi huku kwetu ni pumba za nafaka yaani mahindi mpunga na alizeti Reply
THOMAS KILONGOZI 02/09/2017 17:07:33 PM
mh naomba Fanya kunchek hapa ndugu 0717451818 /0768351802 Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:41:22 AM
Nenda Kamchukue mtalaam Kituoni kwetu Kyela ama wasilaina nasi kwa simu kwa maelezo zaidi (+255) 22 265 0043 Reply
FARAJA MKALATI 15/06/2017 10:24:56 AM
bado hamjatuambia chakula bora ni kipi kwa samaki Reply
SIJA AMOS KABOTA 26/07/2017 04:17:15 AM
NAHITAJI FORMULA YA KUCHANGANYA CHAKULA CHA SAMAKI Reply
UNGANI RAPHAEL 02/01/2017 03:05:37 AM
nahitaji fomulae ya kutengeneza chakula cha kambare Reply
STEPHEN 08/10/2016 09:55:58 AM
nimeanza ufugaji wa samaki kambale mbarali lakini inaonekana ukuaji unaenda kidogo licha kulisha mara mbili mlonge,mupumba ya mahind,mashudu,pumba mpunga wanamiezi miwili sasa Reply
AMON PETER 29/08/2016 11:16:16 AM
kinachanganywa je Reply
UNKNOWN 30/08/2016 03:34:48 AM
mimi ni mfugaji wa samaki nipo Arusha, je hapa mna kituo? Reply
DAVID METHOD 06/10/2016 09:24:27 AM
Niko dar . je ninaweza kupata wapi ushauri wa kitaalam kuusu ufugaji wa samaki? Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:42:03 AM
+255) 22 265 0043 Reply
PHILBERT MTEY 06/02/2016 10:44:04 AM
Mimi nifugaji ninaye anza ufugaji wa samaki,Naomba kujua namna ya kupata chakula bora cha samaki.... Reply
JOHN MSHOTA 01/05/2017 08:54:39 AM
Chakula bora cha samaki ni kipi?mimi kama mfugaji nahitaji kujua. Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:35:48 AM
Njoo Ofisini Kwetu Kunduchi Upate ushauri Bure Reply
HARUNI MASUDI 06/03/2017 06:54:12 AM
HARUNI MASUDI WA MTWARA TANZANIA natamani sana kufuga samaki tangu niko mdogo yaani ufugaji wa samaki kwangu ni ndoto kubwa kwangu lakini japokuwa na mazingira yanayokidhi kwa ufugaji wa samaki, lakini nnachangamoto ya mtaji na nnachokiomba kwa ulioanza shuhuri hii ya ufugaji nawaomba mnijuze gharama za uchimbaji wa bwawa na vipimo bora vya bwawa. Reply
NEEMA JEREMIA 13/03/2017 03:56:51 AM
Kuna kisima nimekijenga kwa ajili ya chemba Ila sijaanza kukitumia kwa sasa natunziaga tu Maji kwa ajili ya matumizi binafsi, je naweza kufugia samaki? Reply
DAUDI CHACHA 23/04/2017 10:11:05 AM
Wazazi wangu ni wafugaji wa samaki kando ya zima Victoria huko musoma mkoa wa mara. Ana mabwawa tisa ya upana wa atua za miguu 20 kwa 32. TATIZO ni kuwa samaki Hawawi wakubwa. Pamoja na kubadili mbegu tofauti. Nadhani chakula ni tatizo. Tupe fomula ya uchanganyaji chakula kabla atujakata tamaa. Reply
BENSON MOHELE 15/08/2018 10:34:35 AM
samahani, ni zipi pembejeo muhimu kwa ufugaji wa samaki kwa mbinu za kisasa.?Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:31:16 AM
muulize mtaalamu at amonshoko@tafiri.go.tz moja kwa moja Reply
SAILALE INNOCENT EDWARD 15/08/2018 10:32:34 AM
Tupo Mwanza Nyegezi, Kigoma, Kyela, SjHirati na Dar es salaam Kunduchi. Karibuni Reply
LINKEDIN TRAINING AMSTERDAM 28/01/2019 09:21:14 AM
I found this blog after a long time which is really helpful to let understand different approaches. I am going to adopt these new point to my career and thankful for this help. visit us-http://linkedintrainingamsterdam.com/Reply
ISAYA MWAFULANGO 19/03/2019 15:59:08 PM
Nawapongeza watafiti kwa lengo la kutupunguzia gharama za ulishaji samaki kwa kutumia rasilimali zinazo patikana maeneo yetu. Naomba kufahamu aina hizo saba za vyakula vilivyotumika kwenye utafiti (Mchanganyiko wake)Reply
STERIUS MASUNGA 22/05/2019 13:55:35 PM
Mimi nina mashine yangu, yakutengeneza chakula cha aina zote za samaki. Maeneo ya bagamoyo, ila tatizo sijui uendeshaji wa mashine hiyo na sifahamu mchanganyiko wa chakula chenyewe je mwaweza kunisaidia namna ya utengenezaji nikafungua duka kubwa la usambazaji wa chakula hapa nchini? Please call me via 0745189046. steriusmasunga@gmail.comReply
JOHN KIMARIO 02/02/2020 09:26:52 AM
Asante kwa chapisho zuri. Naomba kama matokeo ya kazi hii yapo tayari muyaongezee katika kurasa za TAFIRI. Asanteni sanaReply
GABRIEL MASALA 10/07/2020 09:30:16 AM
MTAALAM WA UFUGAJI WA SAMAKI KUTOKA SUA-MOROGORO. Makala hii ni nzuri na ina msaada mkubwa katika swala zima la ufugaji wa samaki. Kwakua zaidi ya 70% za gharama ya uendeshaji wa mradi wa ufugaji wa samaki ni chakula. Hivyo kumpatia mkulima njia ya kupunguza gharama huku akiongeza ubora wa samaki, ni swala bora sana. Hongereni TAFIRI.Reply

Leave your comment here

Your comment will be posted after it is approved.
Name(required)* E-mail(optional)
Comments(required)*
Notify me of new comments to this post by email